Leo hii, tutaangalia uhusiano kati ya Israeli na Marekani. Kwa nini Marekani inamkumbatia sana Israeli, kwenye makala hii nitakupitisha kwenye sababu zote za msingi kujibu swali hilo. Mwaka 1948: Dunia inaanza kutulia baada ya Vita vya Pili vya Kidunia. Palestina, eneo lililokuwa chini ya Waingereza, liko kwenye mvurugo wa vita kati ya Wayahudi na Wapalestina. Mei 14, inatangazwa kuzaliwa kwa nchi ya Israel. Muda mfupi tu baadaye, Marekani inasema: "Tunakubali Israel!" Kwanini haraka hivyo? Sababu ziko Siasa, Imani, na faida za kimataifa.
Vita Baridi:
Baada ya Vita vya Pili, Marekani na Umoja wa Kisovieti zilianza Vita Baridi. Israel, ikiongozwa na demokrasia, ikawa rafiki wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati ambalo Urusi ilitaka kushika. Nchi za Kiarabu kama Misri zilisaidiwa na Urusi, kwa hivyo Marekani ilitumia Israel kama "ngome" ya kuzuia uenezi wa Ukomunisti.
Faida za Kijeshi na Kiuchumi:
Israel ni kituo cha teknolojia ya kijeshi. Inatengeneza mifumo kama Iron Dome inayozuia makombora. Marekani hupata mbinu hizi na habari za kijasusi kutoka kwa Israel. Kwa mfano, baada ya mashambulio ya 11 Septemba, Israel ilisaidia Marekani kujua njia za kuwashinda magaidi.
kiuchumi, Marekani inampa Israel zaidi ya dola bilioni 3.8 kila mwaka kwa silaha. Lakini hela hizi zinarejea Marekani kwa kununua silaha kutoka kwao. Kwa hiyo, ni kama biashara Marekani hupata pesa na kudumisha nguvu ya Israel.
AIPAC:
Mwanzo wa AIPAC: 1950s, Mwaka 1953, baada ya Israel kuanza kutambuliwa na mataifa machache, mwanasheria wa kimarekani Isaiah L. Kenen aliamua kufanya jambo. Kenen alianzisha kikundi kidogo cha AIPAC (American Israel Public Affairs Committee) kwa lengo moja kufanya Marekani iwe rafiki wa karibu wa Israel.
Mwanzoni, AIPAC ilikuwa kama "klabu ya siri." Kenen alitembelea ofisi za wabunge na kuwaelezea, "Israel ni demokrasia pekee Mashariki ya Kati. Msaada wenu utalinda maslahi ya Marekani dhidi ya Umoja wa Kisovieti." Mwaka 1962, AIPAC ilishawishi Congress kuipa Israel msaada wa kwanza wa kijeshi wa dola milioni 13.
Miaka ya 1980: Kuimarika kwa AIPAC.
Miaka ya 1980 ilikuwa "Zama za dhahabu" kwa AIPAC. Wakuu wa kikundi waligundua njia mpya ya kushawishi siasa, kuchangia pesa kwa wagombea wa Congress. Kwa kutumia PAC (Political Action Committee), AIPAC ilianza kutoa mamilioni ya dola kwa wabunge wanaounga mkono Israel. Mwaka 1984, Congress ilipitisha sheria ya kumpa Israel dola bilioni 3 kwa mwaka kwa msaada wa kijeshi. Raisi Ronald Reagan alipinga kiasi hicho.
2015: Vita Dhidi ya Mkataba wa Iran.
Mwaka 2015, Rais Barack Obama alipatana na Iran kuhusu mkataba wa kuzuia silaha za nyuklia. Israel na AIPAC walikasirika. Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel, alikwenda Congress kupitia msaada wa AIPAC na kusema: "Mkataba huu ni hatari!"
AIPAC ilitumia dola milioni 20 kwa matangazo ya kupinga mkataba. Pia, wakapeleka wabunge 330 kukutana na Netanyahu. Matokeo yake, Congress iligawa—wengi wa Republican na baadhi ya Democrats walipinga Obama. Ingawa mkataba ulipitishwa, AIPAC ilionesha uwezo wake.
Miaka ya 2020: AIPAC na Wapinzani.
Mwaka 2022, kikundi kipya cha AIPAC United Democracy Project kilitumia dola milioni 36 kuwashambulia wagombea wanaopinga Israel. Wagombea wengi waliosimama na Wapalestina walishindwa kuchaguliwa.
AIPAC ni "siri" kuu ya uhusiano wa Marekani na Israel, Lakini je, AIPAC itadumu milele? Kwa sasa, bado inatawala, lakini mabadiliko ya siasa ya ndani ya Marekani yanaweza kuvunja nguvu zake. Kwa sasa, Israel na Marekani ni marafiki damudamu," na AIPAC ndiye mshika wa ufunguo wa urafiki huo.
Unaweza pia kuangalia makala hii maalumu kwa nini Marekani inamkumbatia Israel? Sababu zilizojificha. Pia usisahau kutembelea mitandao yetu ya kijamii kila siku ili kujipatia elimu.

0 Comments