Kuhariri picha ni kitu ambacho kinafanyika sanaa unaweza kuhariri picha zako ambazo ulipopiga hazikutoka vizuri, Kabla ya kuziweka katika mitandao yako ya kijamii unaweza ukaongeza vitu kama vile rangi, mwanga n.k kuongeza manjonjo.
Miezi miwili iliyopita niliwahi kuandika kuhusu AI( ATIFICIAL INTELIGENT ) na nikakupa moja ambayo inahusuka na mambo ya Picha, Sasa naona umeanza kujiuliza je ni Application gani ambazo uzitumie... Ziko nyingi, kuna zile ambazo zinauzwa na kuna zile za bure kabisa ni wazi kuwa wengi wetu tunapenda zile za bure sio.
Leo makala hii inakuletea listi ya Application ambazo unaweza ukatumia kuhariri picha zako. Unataka uwe unapost Picha nzuri kuanzia leo kwenye mitandao yako ya kijamii tumia hizi kwani zitakuwa msaada mkubwa kwako.
1. Lightroom
Sasa hii baadhi ya vipengele unaweza ukavipata bure lakini ukitaka kupata vipengele vizuri zaidi itakubidi ulipie kila mwenzi.
Najuwa wengi mshazoea kuiona kwenye Computer ila wanayo pia program ya simu humu utapata kutumia vitu vingi kama mtaalamu na haya yote yatakufanya mwisho wa siku utoke na picha kali sana!
Vitu kama emoji na stika zingine sio kabisa vya kuvitegemea humu lakini mambo mengine mengi tuu unaweza kuyapata, kingine ambacho nimekipenda inakuja na Cloud yake hifadhi ya kimtandao na inakuwezesha kuanza ku’edit kwenye kifaa kimoja na ukamalizia kwenye kingine.
2. Adobe Photoshop Express
Hii haina tofauti kubwa sana na Lightroom lakini swala kama hifadhi ya kimtandao (Cloud) huwezi kupata humu.
Adobe Photoshop Express haina mambo mengi kabisa, ni moja kati ya programu ambayo ni rahisi kabisa kutumia ukiwa unahariri picha zako, ni chaguo zuri kwa watumiaji wote, Android na IOS
Kwa kutumia app hii, ni rahisi sana kuhariri picha! Hii ni kutokana na feature zake zilivyo rahisi kupatikana hamna haja ya kusoma Photoshop kuielewa hi program.
3. PicsArt
Labda usichokifahamu kuhusu PicsArt ni mtandao wa kijamii kama vile Instagram, unaweza piga picha, ukai’edit’ na kui’share katika mtandao huo.
Ina vipengele vinavifanya kazi vizuri, hii inahusisha time laps, collage, effects na features na ina tools nyingi za kutumia ila sasa ubaya ni kwamba lazima utengeneze account ili kutumia feature nyingi, na haitakiwi kutumiwa watu chini ya miaka 13 kutokana na content za kikubwa.
4. BeFunky
Hii ni moja ya programu best kutumia, haswa kwa wanafanya kazi ya kupiga Picha kwani inaongeza uzuri katika picha za potrait, lakini pia ni Photo editor na colage maker alafu uzuri ni kwamba haina ads kati wakati unaitumia hivo kukupa uhuru na muda wa kutosha kuhariri Picha zako.
Ila mbali na uzuri wa app hii naeza kusema wanafelii kwenye tools ili upate nzuri lazima ununuwe na ni rahisi sana kujirudsha nyuma na kupoteza Picha ilivo edit.

0 Comments