Ni wazi kuwa wote tunatumia internet hata unaposoma makala hii unatumia Internet ndio mana leo nimependa kukuandikia kuhusu matumizi bora na salama ya Internet.
Intaneti ni kiungo muhimu sana katika ulimwengu wa teknolojia katika kuwezesha mambo mbalimbali ambayo yanahitaji kuwasiliana lakini kuna wakati inabidi mawasilano hayo yawe ya siri na salama.Unataka kuficha utambulisho wako ukiwa mtandaoni? Je unataka usiache alama (digital footprint) pale unapotumia mitandao?. Sasa hapo ndio VPN inapokuwa muhimu sana.
VPN ni kifupi cha "Virtual Private Network," Kwa kiswahili ni mtandao wa kibinafsi wa kidigitali ni mfumo wa teknolojia unaojenga uhusiano salama na mtandao kutoka kifaa chako hadi seva iliyoko mahali pengine. Hii inasaidia kuongeza faragha na usalama wako mtandaoni kwa kusafirisha data kupitia njia iliyofichwa.
Je ushawahi kuuliza unaweza kupenya vipi na kuingia site ambazo zimefungiwa kwa nchi yako?. Basi jibu ni kupitia VPN, hata baadhi ya mitandao na internet ikizimwa nchini kwako, basi VPN itakusaidia kupata huduma ya internet bila shida yoyote ile.
China na baadhi nchi za kiarabu kuna baadhi ya mitandao imefungwa, ila unaweza kushangaa kuna watu wapo China na wanatumia Whatsapp, basi jibu ni kuwa wanatumia VPN kuficha location ya nchi walipo.
Huko Dark web... wengi wanatumia VPN kwa sababu mtu hataweza kukupata sehemu ulipo wala taarifa zako za kifaa chako.
Ila kumbuka, kuna baadhi nchi kutumia VPN ni kosa kisheria. Kwa mfano Tanzania. Na hii makala nimelenga kutoa elimu tu, na sio kufundisha watu vinginevyo.
Nimeona nikuletee angalau VPN 5 ambazo ni bora na ningependa uwe unazitumia Ili kukulinda na kukufanya uwe salama pale unapokuwa mtandaoni.
1.Betternet
Nakufungulia orodha na moja ya chaguo, linalopendwa na watumiaji wengi duniani kote; Betternet. Moja ya sababu za mafanikio yake ni ulinzi mzuri, inapatikana kwa kila aina ya vifaa na inaweza kudanlodiwa kwenye iOS, Android, PC au Mac. Pia ina site zake kwenye Chrome au Firefox.
Jambo kuu la Betternet ni hilo na haina data au vikwazo vya kasi. Pamoja na hayo, ni lazima nikuambie kwamba haihitaji aina yoyote ya usajili ili kuweza kuitumia. Na ni bure kabisa kutumia VPN hii.
2. ExpressVPN
Kwenye orodha yangu hii ni VPN ya pili na ni mojawapo ya programu bora za VPN ambazo lazima ujaribu mara moja. Hii ni kwa sababu huduma ya VPN ni ya haraka sana na haiingizi data ya watumiaji. Jambo la kuvutia kuhusu Express VPN ni kwamba ina seva zaidi ya 145 katika zaidi ya nchi 94.
Na uzuri ni kuwa Inaoana na aina zote za muunganisho wa mtandao, ikijumuisha 4G/LTE, 3G, na Wi-Fi. ExpressVPN ni chaguo zuri kwa mtu yeyote ambaye anataka kuboresha faragha na usalama wake mtandaoni. Pia kwa watu wanaotaka kufikia tovuti au maudhui yaliyozuiwa.
3.Hide.me
Mojawapo ya VPN maarufu za bure duniani, nikueleze kwamba hide.me Inajivunia kuwa "VPN ya haraka zaidi ulimwenguni" na haina haja ya kujisajili.
Na jambo la kuvutia zaidi kuhusu hide.me,
programu yake ya Android ina kitufe cha haraka (Cha kuwezesha VPN) kwenye ukurasa wa nyumbani. Na ni salama kusema kwamba ndiyo VPN ya haraka na bora zaidi ya bure na ni chaguo la kuvutia sana kwa wale wanaotaka kuvinjari mtandao kwa usalama na bila kujulikana.
4.Opera VPN
Sikuweza kuwatenga kutoka kwenye orodha hii Opera VPN, chaguo la haraka na la bure. Opera VPN na huja pamoja na Kivinjari cha Opera.
Lakini tofauti na programu zingine za VPN, haitalinda watumiaji wakati wa kutumia surch engine nyingine kama chrome inaweza kutumika tu kwenye kivinjari cha Opera.
Kwa nini utumie Opera VPN?. Hakuna kikomo cha data na hakuna usajili unaohitajika, hakuna programu tofauti na inafanya kazi ndani ya kivinjari.
5.Proton VPN
Watu mara nyingi hupendekeza VPN zinazolipwa kulingana na imani kwamba hakuna kitu kinachokuja bure. Lakini ProtonVPN inapatikana bure bila ada zozote zilizofichwa, matangazo, vikomo vya data au kuuza data ya watumiaji kwa siri.
Lakini bila shaka, hi si habari njema. ukiamua kutumia ProtonVPN utaweza kutumia kifaa kimoja pekee kwa wakati mmoja. Japo Kuna vipengele zaidi katika programu hii ya bure ya VPN, kama vile: kipengele ambacho huzuia kifaa kuanzisha miunganisho wakati VPN imezimwa kimakosa.
Jambo kuu kuhusu Proton VPN ni kwamba ni bure kabisa kutumia, na inakuja na sera kali ya kutoweka kumbukumbu.
Hizo ni VPN 5 ambazo ni bora na hutoa ufungaji salama wa data zako na kusaidia kuficha anwani yako hivyo kupunguza hatari ya kuvuja kwa taarifa zako binafsi wakati wa kutumia mtandao.
Unaweza pia kusikiliza Episode hii maalumu kuhusu VPN bora za kutumia Ili kukulinda na kukufanya uwe salama pale unapokuwa mtandaoni hapo chini. Pia usisahau kutembelea mitandao yetu ya kijamii kila siku ili kujipatia elimu kuhusu teknolojia.

0 Comments