Artificial Intelligence (AI) ni nini?

 Artificial Intelligence (AI) ni nini?

Kama ni mfuatiliaji wa mambo yanayohusu Teknolojia ni rahisi kuwa umeshakutana na neno Artificial Intelligence au AI tunaweza kusema "Akili bandia" kwa kiswahili kwenye ulimwengu wa technolojia kwa sasa Artificial Intelligence ni moja kati ya mambo yanayosikika sana.

AI ni matumizi teknolojia yanayowezesha kompyuta au mashine kufanya mambo ambayo kwa kawaida huhitaji kutumia uwezo wa kiakili kama binadamu kwa mfano kutambua vitu, watu, lugha, sauti, kufanya maamuzi, kutabiri, kutafsiri, kujifunza.. nk

Unaposikia Artificial Intelligence unaweza kuadhani hii inahusika tu maroboti na teknolojia za hali ya juu ambazo hujawahi na hutawahi kuzitumia katika maisha yako.

Artificial Intelligence pia inatumika katika teknolojia nyingi za kawaida zinatumiwa na watu wengi katika maisha ya kila siku ingawa pia hutumika kwenye maroboti na teknolojia nyingine kubwa za hali ya juu.

Sasa ngoja nikupe AI bora ambazo unatakiwa kuzifahamu na kuzitumia katika matumizi mbalimbali ambayo unafanya mtandaoni.

1.Chat GPT
Chat GPT ni Ai ilioanzishwa na OpenAI,
Ikiwa ni moja mifumo ya GPT (Generative Pre-trained Transformer). AI hii ina uwezo wa kutoa majibu kwa maswali ambayo utayauliza na kuendeleza mazungumzo, imekuwa na matumizi katika maeneo mbalimbali kama vile kuboresha huduma za wateja, kusaidia kazi za kimtandao, kutoa ushauri, na kufanya majukumu mengine yanayohusiana na lugha. Pia, mfano huu umekuwa na jukumu muhimu katika kuboresha mawasiliano na uzoefu wa watumiaji kwenye tovuti na programu mbalimbali.

2. Adobe Firefly
Adobe ni moja kati ya programu kubwa sana za kuhariri picha au kutengeneza kabisa picha kwa muonekano ambao wewe unautaka, ukiachana na maswala ya picha bado kuna vitu vingi inaweza kufanya kama vile kuandaa nembo n.k

Lakini pia wamekuja na AI (Artificial Inteligency) Adobe firefly programu kubwa ambayo utaweza itumia katika maswala mazima ya kuhariri picha kitu ambacho teknolojia hii itafanya ni kuhakikisha kuwa inafanya kazi ambayo umeiamuru wewe kumbuka tuu kwamba kwa zamani ilibidi kazi hiyo uifanye wewe.


3. Durable.co
AI inakusaidia kutengene tovuti nzima na picha na nakala kwa sekunde, kwa wale wenye makampuni au biashara na taasisi mbalimbali AI hii itakupa uwezo kutengeneza tovuti iliyoundwa kikamilifu iliyo na nakala, picha na fomu ya mawasiliano ndani ya dakika moja na kukupa uwezo wa kubadilisha tovuti yako kwa urahisi.
Kama tunavofahamu blogs ni muhimu kwa mashirika yetu ili kuwezesha watu kuangalia shughuli mbalimbali zunazofanywa.

4. Dreamix.ai
Itakusaidia kuziona na kupata picha nzuri zinazozalishwa na AI. Sasa kwa wale wanaofanya graphics na editing ya video au picha AI hii itakusaidia wewe kupata picha ya aina yoyote ile.
Mfano untaka kupata mtu aliyeketi kwenye nyasi, au unataka kupata ngombe anaevuta sigara basi AI hii itakuletea kwa haraka bila ya kupoteza muda walo.

5.breeze.ai 
AI hii itakusaidia kuunda picha za bidhaa kwa sekunde inaweza kukupatia Picha za ubora wa juu ili kuzitumia kwa watu na unaweza pata picha za kushangaza kwa matumizi yako ya kila siku kwa mitandao ya kijamii, na shughuli za graphics.
Na hii kwa wafanyabiashara inaweza kuwa nzuri kwao kwani itawasaidia kutengeneza picha za products mbalimbali wanazozitaka na wanaweza kuchapisha moja kwa moja picha hizo kwenye mitandao ya kijamii kama vile Instagram, Facebook, na Twitter.

Natumaini mpaka hapa utakuwa umeelewa kuhusu AI Artificial intelligence za kutumia kurahisisha mambo mbalimbali unayofanya kila siku.

Unaweza pia kusikiliza Episode hii maalumu kuhusu AI Artificial intelligence za kutumia Ili kurahisisha shughuli zako mbalimbali hapo chini. Pia usisahau kutembelea mitandao yetu ya kijamii kila siku ili kujipatia elimu kuhusu teknolojia.

Post a Comment

0 Comments