![]() |
| Fata njia hizi kulinda Simu na Laptop yako dhidi ya Wadukuzi. |
Kuingia mtandaoni haimaanishi tu kwamba tunaingia katika ulimwengu wa fursa zisizo na mwisho, starehe au furaha.
Badala yake, inamaanisha pia kwamba tunafanya maisha yetu yawe wazi kwa watu tusiowajua na watu wanaoweza kutudhuru.
Mara nyingi, watu wanadukuwa ili kuiba taarifa, kudhibiti akaunti, au kusababisha madhara kwa mfumo au taasisi.
Leo katika Makala hii nataka nikupe hatua kadhaa unazoweza kuchukua ili kuepuka kudukuliwa kwenye simu na laptop yako.
1. Fanya update ya software na appllication zako,
Akuna simu isiyopokea appllication toleo jipya la security pale tu watengenezaji wanapoachia hivyo hakikisha unafanya update ya appllication zako kupitia soko la play store au software kupitia setting utakua salama, mara nyingi update izi huwa zinakuja Ili kuboresha ufanyaji kazi na hujumuisha udhibiti wa usalama ulioboreshwa.
2. Tumia namba ya Siri ambayo ni ngumu,
kwenye orodha yangu hili ni jambo la pili ambalo ningependa ulizingatie tumia namba ya siri ngumu kwa vifaa vyako vyote. Ni bora kutumia mchanganyiko wa herufi kubwa na ndogo, nambari, na alama. Epuka kutumia password zinazoweza kutambulika kirahisi, kwani hiyo itatowa urahisi wa kudukuliwa Kwa taarifa zako
Jambo la kushangaza ni kwamba Mark Zuckerberg alitumia neno la siri ‘dadada’ kwenye akaunti zake za mtandao.
Salama sana, sawa? Ukitaka password ngumu tumia Alphanumeric maana kuwa neno yana herufi kubwa na ndogo, na namba zilizochanganyika n.k. hi ni njia bora ya kuzuia udukuzi.
3. Clear cookies on your browser,
Futa history zote kwenye browser unayopenda kutumia mara kwa mara kwani Cookies izi ni baadhi ya information zinazokuwa stored kwenye kifaa chako pale ambapo unakuwa unaperuzi mtandaoni sasa hizi husaidia tovuti kukumbuka wewe ni nani, kwa hivyo, Ili kuweza kukupa kwa urahisi vile unavovitaka lakini sasa wadukuzi wanaweza kutumia history hizo ili kupata information zako.
4. Sikuweza kuwatenga na hili jambo Epuka free WiFi,
Aliyesema cha bure kina gharama hakukosea hivvo ukitaka kuwa salama jitaidi sana na jiepushe kujiunga na mitandao ya Wi-Fi isiyojulikana au ya umma bila kulinda data yako. Tumia mitandao salama na kama inahitajika, Kwa ulazima sana basi tumia huduma ya VPN kwa kuongeza usimamizi wa data na kupunguza hacker kudukuwa taarifa zako.
5. Hakikisha kuwa tovuti ni salama unapoingiza taarifa zako,
Mara nyingi unapokuwa mtandaoni jihakikishie na tovuti unayoweka taarifa zako za faragha kwani unaweza kuweka taarifa kwenye tovuti wanazotumia ma hacker ivo kuwapa urahisi wa kupata taarifa zako, usipende kufunguwa kila link unayotumiwa au file za unazotimiwa Bila ya taarifa nazo kwani inaweza kuwa njiaa ya udukuzi,
Naimani Kwa kufata mambo aya na kuwa makini na tabia yako ya mtandaoni, utasaidia kulinda simu yako na kompyuta dhidi ya hatari za kudukuliwa au kutowa information ambazo uzitaki.
Unaweza pia kusikiliza Episode hii maalumu kuhusu hatua kadhaa unazoweza kuchukua ili kuepuka kudukuliwa kwenye simu na laptop yako hapo chini. Pia usisahau kutembelea mitandao yetu ya kijamii kila siku ili kujipatia elimu kuhusu teknolojia.

0 Comments