![]() |
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina sheria na kanuni zinazosimamia matumizi ya mtandao na makosa ya kimtandao. Kufanya makosa ya kimtandao kunaweza kusababisha kushtakiwa na kuadhibiwa kulingana na sheria zilizopo.
Makosa hayo ya kimtandao yanaweza kusababisha mashtaka na adhabu ya faini na kujikuta ukipoteza Pesa zako au ata kwenda jela kwa miaka kadhaaa hasa tukilenga mfano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa hiyo, jiunge nami katika makala ya leo aya ni makosa Tano ya kimtandao yanayoweza kusababisha mashtaka nchini Tanzania.
1. Udukuzi wa Mtandao (Hacking) Kuingilia kwa njia haramu katika mfumo wa kompyuta au akaunti za watumiaji kunaweza kusababisha mashtaka chini ya Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, kutaka kujuwa mambo ambayo mtu anayafanya mtandaoni, au kujuwa sms zake anaongea na nani iyo yote ni makosa ya udukuzi na unaweza ukashitakiwa kwa kosa hilo.
2. Kutuma au Kusambaza Ujumbe wa Chuki (Cyberbullying): Kutuma ujumbe wa chuki au kashfa mtandaoni kunaweza kusababisha mashtaka kulingana na sheria za kashfa au sheria za makosa ya kimtandao, au kujaribu kuwapotosha watu kwa kutuma barua pepe za udanganyifu au kuanzisha tovuti bandia kunaweza kusababisha mashtaka chini ya sheria zinazohusiana na udanganyifu.
3. Uvamizi wa Faragha (Privacy Invasion) Kuchapisha au kusambaza taarifa za kibinafsi au picha za watu bila idhini yao kunaweza kusababisha mashtaka chini ya sheria za faragha, 😂😂 jiulize je ni marangapi umekuwa ukipost picha za wenzako bila idhini yao hivo ukitakiwa uwe umeshashitakiwa najuwa huenda ulikuwa ujui kama unafanya kosa ila leo nimeshakufahamisha.
4. Ukiukwaji wa Hakimiliki (Copyright Infringement) Kuchapisha au kusambaza yaliyomo ambayo ni kinyume cha hakimiliki bila idhini ya mmiliki wa hakimiliki kunaweza kusababisha mashtaka chini ya sheria za hakimiliki, na hii iko pana zaidi kutumia chochote mtandaoni ambacho kina hakimiliki ni kosa kubwa.
5. Kutoa Vitisho Mtandaoni (Online Threats): Kutoa vitisho au kusababisha hofu mtandaoni kunaweza kusababisha mashtaka kwa kukiuka amani na utulivu, hii yote inahusiana ka kushawishi watu au kutishia amani ya watu au mtu binafsi mtandaoni hivo kwenye Sheria kipo kifungu ambacho unaweza kuhukumiwa.
Ni muhimu kuzingatia sheria na kanuni za mtandao zinazohusika katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuheshimu haki za wengine ili kuepuka kushtakiwa na kuadhibiwa kwa makosa ya kimtandao.
Je, kuna sharia yoyote uliyokua unavunja bila ya wewe mwenyewe kujua? Kama ipo natumaini mpaka sasa umeshafahamu kwamba ni kosa na kuna adhabu kali sana kutolewa endapo mtu atabainika na makosa haya.
Unaweza kusikiliza episode maalumu kuhusu makosa ya kimtandao hapo chini. Pia usisahau kutembelea mitandao yetu ya kijamii kila siku ili kujipatia elimu kuhusu teknolojia.

0 Comments