Ujumuishi Mtandaoni: Umuhimu, Ulinzi na Faida Yake.

Takwimu za mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA, zinaonyesha kuwa watumiaji wa intaneti wanaongezeka kwa kasi kubwa sana nchini Tanzania mpaka kufikia watumiaji 34,469,022 kwa mwaka 2023 kutoka watumiaji 23,808,942 kwa mwaka 2018 kukiwa na ongezeko la watumiaji 10,660,080 ndani ya miaka mitano, Licha ya kuwa na ongezeko kubwa la watumiaji wa Intaneti kati ya watumiaji hao ni asilimia ndogo sana wanaojua namna ya kutumia intaneti kwa usahihi na manufaa zaidi. Kwanini wengine wameachwa nyuma kwenye matumizi ya mitandao ya kijamii? usalama wa watumiaji upo vipi? Makala hii, imeainisha mambo mbalimbali kuhusu ujumuishi mtandaoni. Chukua muda wako kutazama video iliyobeba elimu iliyojitosheleza kuhusu ujumuishi mtandaoni.

Imeandaliwa na Edward Mbaga


Post a Comment

0 Comments