Cyber security Tanzania: kujilinda dhidi ya Vitisho vya Kimtandao


Vipi umeshawahi kukutana na ujumbe mfupi wa TUMA KWA NAMBA HII au SAMBAZA UJUMBE HUU KWA WATU 20 UJISHINDIE KIASI FULANI CHA FEDHA?  Waswahili wanasema maneno haya si mageni jijini labda kwa wageni wa mambo haya….

Katika miaka ya hivi karibuni, wizi wa kimtandao umeongezeka kwa kasi nchini Tanzania. Ingawa serikali na mashirika mbalimbali yamejitahidi kutoa elimu kuhusu usalama mtandaoni, wengi bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu jinsi ya kujilinda na vitisho vya kimtandao. Watu wengi wanakumbwa na matatizo kama vile wizi wa fedha kupitia huduma za simu za kiganjani, udukuzi wa akaunti za mitandao ya kijamii, na kupoteza taarifa zao za kibinafsi kutokana na udhaifu wa usalama mtandaoni.

Mambo ya msingi katika ulinzi wa kimtandao ni kufahamu hatari, kuchukua tahadhari, na kuwa na maarifa ya kuboresha usalama wa taarifa zako.

Hii ni mifano halisi ya vitisho vya kimtandao na hatua za kujilinda:

1. WIZI WA KIFEDHA KUPITIA SIMU ZA KIGANJANI

Wizi wa kifedha kupitia huduma za simu za kiganjani kama M-Pesa umekuwa changamoto kubwa nchini Tanzania. Wahalifu hutumia mbinu za "SIM swap" na "phishing" kuiba fedha za wateja. Katika "SIM swap," mhalifu hutumia taarifa za kibinafsi, kama picha ya kitambulisho, ili kubadili namba ya simu ya mwathirika na kisha kutumia akaunti za kifedha kutuma fedha kwa urahisi.

Kwa Mujibu wa Ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya mwaka2022 ilionyesha kwamba wizi wa fedha kupitia huduma za simu za kiganjani uliongezeka kwa asilimia 15. Watu wengi walikuwa wahanga wa mashambulizi haya kwa sababu ya kutokujua hatari zinazohusiana na matumizi ya simu za kiganjani.

 

2. PHISHING NA WA AKAUNTI ZA SOCIAL MEDIA UDUKUZI

Udukuzi wa akaunti za mitandao ya kijamii, kama Facebook na Instagram, umeendelea kuwa tatizo kubwa. Wahalifu hutuma viunganishi vya udukuzi au barua pepe zinazojifanya taasisi halali, kama benki au huduma za kibenki, ili kupata taarifa binafasi za akaunti, kuiba fedha au kutumia taarifa hizo kwa madhumuni ya uhalifu. Kupitia Ripoti ya Tanzania Communications Regulatory   Authority (TCRA) ya mwaka 2021 ilionyesha kwa Watanzania wengi walikubali kutoa taarifa zao za kifedha kwa njia za kimtandao, jambo ambalo lilisababisha wizi mkubwa wa fedha na taarifa za kibinafsi.

 

3. ULINZI WA TAARIFA ZA KIBINAFSI NA DATA

Kama ilivyo katika maeneo mengine duniani, ulinzi wa taarifa za kibinafsi ni suala nyeti. Watu wengi wanatumia huduma za mtandao bila kuchukua tahadhari ya kutosha, kama kutumia nywila au namba za siri dhaifu au kutohakikisha usalama wa akaunti zao kwa kutumia teknolojia za kisasa za ulinzi.

Kwa mujibu wa Utafiti uliofanywa na Cyber Security Tanzania (CST)  mwaka 2023 ulionyesha asilimia 70 ya Watanzania hutumia nywila (PASSWORD) kama vile "12345” hali inayowaweka katika mashambulizi ya kimtandao kama vile "brute force attacks."

 

4. MIKAKATI YA KUJILINDA

• Matumizi ya Vidhibiti vya Uthibitishaji wa Wawili (Two-Factor Authentication): Hii ni njia muhimu ya kuongeza usalama wa akaunti zako za mitandao ya kijamii na huduma za kifedha. Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) ilibainisha kwamba matumizi ya uthibitishaji wa wawili (2FA) ni mbinu bora ya kupunguza hatari ya udukuzi.

• Elimu ya Cyber Security kupitia Kampeni ya Cyber Security Awareness ambayo ilianzishwa na serikali ya Tanzania ili kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa ulinzi wa kimtandao. Elimu hii inasaidia kuongeza uelewa kuhusu hatari zinazohusiana na matumizi ya mitandao ya kijamii na huduma za kifedha mtandaoni.

Ulinzi wa taarifa zako ni jukumu letu sote. Hata kama serikali na mashirika ya teknolojia yanaendelea kutoa elimu na mikakati ya kujilinda, kila mmoja wetu anapaswa kuwa na jukumu la kujua hatari za kimtandao na kuchukua hatua za kujilinda. Kwa kutumia mikakati ya usalama kama uthibitishaji wa wawili, kuepuka viunganishi vya udukuzi, na kutumia nywila ngumu, tunaweza kupunguza madhara ya vitisho vya kimtandao. Ulinzi wa kimtandao siyo tu jukumu la mashirika na serikali; ni jukumu letu sote.

Post a Comment

0 Comments