Kuna wewe, na wewe mwingine ndani yako.





Pale tu utakapozaliwa, unapewa majina utakayotumia maisha yako yote. Unarithishwa na dini kutoka kwa wazazi wako.


Ukikua, unapelekwa shule. Hapa utafundishwa na kulishwa vitu vya duniani jinsi vilivyo. Unapata uelewa wa vitu, hili sio tatizo.

Tatizo linakuja pale utakapoamini na kuishi na vitu ulivyoaminishwa ni WEWE.

Wengi wetu ni kama tumechaguliwa jinsi ya kuishi na vitu vilivyotuzunguka au kurithishwa. Ni kama tumefungwa, na kwa bahati mbaya sana tumeshindwa kujitafuta na kugundua SISI ni nani.

Mimi ni nani? nimekuja duniani kufanya nini?. Ni maswali ya kujiuliza.

Mimi ni Leonce, ni jina nililopewa na wazee wangu. Maisha yangu yote nimeishi nikiamini mimi ni Leonce. Hivi siwezi kuwa Abdullah?.

Naishi nikiamini mimi ni mwandishi wa habari sababu nimesoma na nimepewa degree ya mambo ya habari. Ni nini kinachonizuia nisiwe rubani au Engineer?.

Ninawaza tu. Dunia ya sasa ya utandawazi unaweza kuwa mtu yeyote yule. Kuna "Platform" ya kitu chochote unachotaka kujifunza. Usiogope kutoka kwenye WEWE unayejijua. Jitafute WEWE unayetaka kuwa.

Wengi wetu sio SISI, ila tunaishi kutokana na vile wazazi wanavyopenda tuwe, au jamii ilivyotupangia tuwe. Hongera kwa wote waliokataa utumwa huu na kuishi kama WAO.

Bado hujachelewa, unaweza kuwa WEWE kwa kusikiliza ile sauti inayokuita ndani yako. Kama umesomea ualimu, haimaanishi ufe uking'ang'ana kuwa mwalimu. 2022 fuata wito wako.

Nimeandika tu, hata mimi mwenyewe sijijui ni nani 😂.

Post a Comment

0 Comments